Dunia imekuwa na amani zaidi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009 kulingana na ripoti ya Taasisi ya Uchumi na Amani (Global Peace Index) (GPI) iliyotolewa hivi karibuni.
Taarifa
iliyotolewa na Taasisi hiyo (GPI) inaonesha hali ya Amani kuimalika kwa
mwaka huu, ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita ambayo ilionesha
kupungua kwa amani Duniani. Katika Taarifa hiyo
inaonesha, nchi ya Iceland imeongoza kwa mara nyingine tena kuwa nchi
yenye amani zaidi duniani, ikifuatiwa na Denmark na New Zealand. Syria
imeonekana kuporomoka kwa nafasi 30 zaidi na kuwa katika nafasi ya 147.
Katika
Taarifa hiyo Tanzania imepanda kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 56
iliokuwa inashikilia mwaka jana 2011 hadi nafasi ya 55 mwaka huu ikiwa
na alama 1.873. huku ikishika nafasi ya 9 kwa Afrika nyuma ya Morroco
(54), Lesotho (53), na Sierra leone(52), wakati nafasi ya kwanza
ikiongozwa na Botswana (31), Mozambique (48), Namibia(49), Ghana (50) na
Zambia (51).
Nchi zingine za Afrika mashariki ni Uganda (98), Rwanda (119) Kenya (120) , na Burundi (138).
Taarifa
hiyo inaonesha nchi za Syria, Misri, Tunisia, na Malawi zimeporomoka
kwa nafasi nyingi kutoka nafasi zilizokua zinashikilia mwaka uliopita.
huku malawi ikishuka kutoka nafasi ya 39 hadi 60.









