Kurasa za MAISHA

Kurasa za MAISHA blogs

Saturday, August 11, 2012

ORODHA YA NCHI ZILIZO NA ZISIZOKUA NA AMANI - RIPOTI 2012

Dunia imekuwa na amani zaidi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009  kulingana na ripoti ya Taasisi ya Uchumi na Amani (Global Peace Index) (GPI) iliyotolewa hivi karibuni.  

Taarifa iliyotolewa na Taasisi hiyo (GPI) inaonesha hali ya Amani kuimalika kwa mwaka huu, ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita ambayo ilionesha kupungua kwa amani Duniani. Katika Taarifa hiyo inaonesha, nchi ya Iceland imeongoza kwa mara nyingine tena kuwa nchi yenye amani zaidi duniani, ikifuatiwa na Denmark na New Zealand. Syria imeonekana kuporomoka kwa nafasi 30 zaidi na kuwa katika nafasi ya 147.

Katika Taarifa hiyo Tanzania imepanda kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 56 iliokuwa inashikilia mwaka jana 2011 hadi nafasi ya 55 mwaka huu ikiwa na alama 1.873. huku ikishika nafasi ya  9 kwa Afrika nyuma ya Morroco (54), Lesotho (53), na Sierra leone(52), wakati nafasi ya kwanza ikiongozwa na Botswana (31), Mozambique (48), Namibia(49), Ghana (50) na Zambia (51).
Iceland

Nchi zingine za Afrika mashariki ni Uganda (98), Rwanda (119) Kenya  (120) , na Burundi (138).

Taarifa hiyo inaonesha nchi za Syria, Misri, Tunisia, na Malawi zimeporomoka kwa nafasi nyingi kutoka nafasi zilizokua zinashikilia mwaka uliopita.  huku malawi ikishuka kutoka nafasi ya 39 hadi 60.
Somalia










Nchi zinazoshika nafasi za mwisho ni Pakistan, Israeli, Jamhuri ya Afrika ya kati, Korea Korea ya Kaskazini, Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Iraq, Sudan, Afghanistan na Somalia, ambayo ndiyo inashikilia nafasi ya mwisho ikiwa katika nafafi ya 158 .

No comments:

Post a Comment